Kuelekea michuano ya AFCON 2027 Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetia saini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu mkoani Arusha, ambao utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki elfu thelathini, na utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 286.
Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa na Mkandarasi China Southwest Architectural Design and Research Institute Corp. Ltd atakayejenga Uwanja huo.
Waziri wa Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Dkt Damas Ndumbaro amenukuliwa akisema
"Uwanja utazinduliwa na kuanza kutumika rasmi mwaka 2027 wakati wa michuano ya Afcon na utakuwa na majukwaa mawili maalumu,upande mmoja utatumiwa na viongozi wa serikali na upande mwingine utatumiwa na wageni maalumu wasio wa kiserikali, uwanja utakuwa na kumbi mbalimbali,ofisi na maktaba ,Uwanja utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000"
"Tunataka uwanja utumike kwa shughuli za kila siku na si kwa sababu ya mechi tu,Raisi Samia anakuwa raisi wa pili kujenga uwanja mkubwa baada ya ule wa benjamini mkapa uliojengwa na raisi wa awamu ya tatu na uwanja huu utaitwa UWANJA WA SAMIA SULUHU HASSAN"
0 Comments