advertise with us

ADVERTISE HERE

SAHAU KUHUSU MO SALAH MWAMBA HUYU HAPA ALIYEWAPELEKA MISRI ROBO FAINALI

Sahau kuhusu Mohammed Salah pale Ivory Coast kuna huyu bwana mkubwa wa kuitwa Mustafa Mohammed anayekipiga Nantes pale Ligue 1 Ufaransa. Huyu ndiye mchezaji hatari zaidi katika kikosi cha Egypt kwenye michuano inayoendelea .

Mpaka sasa nyota huyu amefunga mabao 3 katika michezo mitatu aliyocheza hatua ya makundi na mabao yake yameisaidia Misri kutinga hatua ya robo fainali kibabe.

Nyota huyu anawania Kiatu cha Ufungaji Bora akiwa na mabao 3 huku mfungaji anayeongoza mbio hizo ni Emilio Nsue Lopez wa Equatorial Guinea.

Mchezo wa kwanza kati ya Misri dhidi ya Cape Verde  ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 nyota huyu alitupia bAo dakika ya 4 ya mchezo huo.

Mchezo wa pili dhidi ya Ghana uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 nyota huyu alitupia bao moja la Misri 

Mchezo wa mwisho dhidi ya Mozambique uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 nyota huyu alifanikiwa kufunga dakika ya 90+3 na kuisaidia timu yake kuingia hatua ya robo fainali .

Katika kundi B ni Cape Verde pekee amefanikiwa kushinda mechi 2 na sare 1 wakijikusanyia point 7 ,Misri wao wamemaliza nafasi ya pili wakiwa na pointi 3 na michezo yote wamesuluhu.Ghana wamemaliza michuano hiyo wakiwa na pointi 2 baada ya kusare Michezo 2 na kufungwa mmoja .Mozambique wao wamepata sare 2 na kufungwa mchezo mmoja.

Haya hapa matokeo ya Misri hatua ya makundi
Post a Comment

0 Comments