BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU HAPA MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA HATTRICK AFCON2023

 Nyota wa Emilio Nsue Lopez kutoka taifa la Equatorial Guinea ndiye wachezaji wa kwanza kufunga Hattrick katika michuano ya AFCON 2023 inayoendelea nchini Ivory Coast.

Nyota huyu amefanikiwa kufunga mabao hayo dakika za 21,46 na 61 akiisaidia timu yake kuondoka na point zote 3 kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Guinea Bissau.

Je Emilio Nsue ni nani

Nyota huyu alizaliwa mwaka 1989 nchini Hispania na mwaka 2004 alijiunga na timu ya vijana ya Mallorca kisha kupandishwa mpaka Mallorca B na baadae timu ya wakubwa ya Mallorca.

Nyota huyu anayecheza katika nafasi za beki wa kulia na winga amekwishawahi kuvitumikia vilabu kadhaa kama Real Sociedad ,Birmingham city, Apoel na sasa yupo Intercity akicheza michezo 42 na kufunga mabao 9.

Kipi kilimrudisha Equatorial Guinea

Emilio Nsue Lopez alizaliwa Hispania na alianza maisha ya soka mwaka 2005 akiitumikia timu ya taifa Hispania chini ya miaka 16 mpaka mwaka 2011 alishachezea timu zote za vijana akicheza michezo 61 na kufunga mabao 20 .

Mwaka 2013 aliamua kurejea  katika taifa la Equatorial Guinea  baada ya kushindwa kupata nafasi katika timu ya taifa ya Hispania .

Akiwa ndani ya jezi ya Equatorial Gu

Baba mzazi wa Nsue Lopez ni mhispania na mama yake ni raia wa Equatorial Guinea na alihamia nchini humo mwaka 1988 alikokutana na mzee Lopez.

Itaendelea......


Post a Comment

0 Comments