Jina la mshambuliaji Emilio Nsue Lopez limeendelea kung'ara nchini Ivory Coast baada ya kufunga mabao mawili kati ya manne yaliyofungwa na Equatorial Guinea dhidi ya Ivory Coast mchezo wa tatu kwa hatua ya makundi.
Nsue Lopez alifunga bao lake la kwanza dakika ya 42 na dakika ya 75 aliandikisha bao la pili na kumfanya nyota huyo kufikisha mabao 5 katika michezo mitatu ya hatua ya makundi akiisaidia timu yake kufikisha pointi 7 na kuongoza kundi lililokuwa na timu za Ivory Coast,Nigeria,Equatorial Guinea na Guinea Bissau.
Mpaka sasa Emilio Nsue ndiye kinara wa ufungaji katika michuano hiyo akiwa na mabao matano na amefanikiwa kuibuka mchezaji Bora wa michezo miwili.
Itaendelea
0 Comments