Mashabiki wa klabu ya Yanga wamejawa na furaha baada ya timu hiyo kupangwa kundi D lenye bingwa mtetezi klabu ya Al Ahly ya Misri
Katika Droo hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezeshwa leo Oktoba 6, 2023 na Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika (CAF), klabu ya Yanga kutoka Tanzania imepangwa kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, Medeama ya Ghana na CR Belouizdad ya Algeria.
Kwa kipindi cha hivi karibuni Yanga wamekuwa na kiwango kizuri baada ya kucheza michezo minne ya ligi kuu NBC wakishinda mechi 3 na kufungwa mchezo mmoja.
Kwa upande wa kimataifa yanga imekuwa na mwendelezo mzuri baada ya kushinda michezo minne ya hatua za awali iliyowapeleka hatua ya makundi baada ya miaka 25
Yanga wanaamini watapata matokeo katika mechi dhidi ya Al Ahly kwa sababu wanakikosi chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini pia mwalimu Miguel Gamondi atapata nafasi ya kuwaona Al Ahly tarehe 20 oktoba watakapovaana na wapinzani wao wa jadi Simba kwenye michuano mipya ya African Super League mchezo utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa hivyo kujiandaa vyema na hatua ya makundi kwani watawasoma wapinzani wao kwa Wepesi zaidi
0 Comments