Yakiwa yamebakia masaa machache kufungwa kwa dirisha la usajili Barani Ulaya Klabu ya Manchester United inakwenda kuwapa furaha mashabiki wake kwa usajili wa kiungo mMorocco Sufian Amrabat.
Nyota huyo anayekipiga klabu ya Fiorentina ya Italy aliingia katika rada za vilabu mbalimbali barani ulaya lakini Chaguo lake lilikuwa Manchester United na sasa dili hilo linakwenda kukamilika baada ya pande zote mbili za vilabu kukubaliana.Amrabat anayecheza nafasi ya kiungo atakwenda kuungana na Christian Eriksen,Bruno Fernandez,Scott Mctomminay,Sancho na Casemiro. Kuingia kwa nyota huyo ni maboresho ya kikosi cha Manchester United chenye malengo ya kutwaa ubingwa wa ulaya na Ligi ya Uingereza kwa msimu wa 2023/24.
Asubuhi ya leo Manchester United ilifanikiwa Kumnasa kwa mkopo beki Sergio kutoka Tottenham na kocha Erik Ten hag anasema nyota huyo ameshaanza mazoezi Carrington na atakuwepo katika mchezo dhidi ya Arsenal siku ya jumapili kuziba nafasi ya Luke show aliyepata majeraha na atakosekana kwa wiki 10.
0 Comments