advertise with us

ADVERTISE HERE

HUYU HAPA BEKI MPYA WA MANCHESTER UNITED

 Klabu ya Manchester United imepadili gia angani  baada ya kushindwa kumnasa beki wa kushoto wa Chelsea Marc Cucurella na sasa wanaangalia uezekano wa kumsajili Sergio Reguilon anayekipiga TOTTENHAM 

Yakiwa yamesalia masaa kadhaa kwa dirisha kubwa la usajili kufungwa ,manchester united imeonyesha nia ya kumsajili nyota huyo kwa mkopo ili kujinusulu kwa kumkosa beki wake wa kushoto Luke show anayesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Luke Show atakuwa nje ya kikosi cha Manchester United kwa muda wa wiki 10 huku mbadala wake Tyrell Malacia akisumbuliwa na majeraha hivyo kumlazimu kukaa nje ya dimba kwa wiki kadhaa.

Taarifa za awali zinasema Manchester united ilipeleka ofa ya paundi milioni 2 kama ada ya usajili wa mkopo kwa Chelsea ili kumnasa Cucurela lakini ofa hiyo ilikataliwa na klabu hiyo kusema nyota huyo thamani yake ni paundi milion 7.

Sergio Reguilon alijiunga na Totenham msimu wa 2020/21akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milion 32 na aliichezea klabu hiyo mechi 52 kabla ya kutolewa kwa mkopo msimu wa 2022/23 kwenda Atletico Madrid alikocheza mechi 11 pekee .

Manchester United wanaamini usajili huo utaimarisha ulinzi kwenye kikosi chao kwa msimu wa 2023/24 wakiwa na malengo makubwa ya kutwaa mataji ya ligikuu ,EFL,FA na UEFA.

Post a Comment

0 Comments