Baada ya tetesi kusambaa kuhusiana na usajili wa nyota kutoka Wolves Matheus Nunez kwa dau pa paundi milion 52 n kuzua maswali kwa wadau wa soka hasa mashabiki wa Manchester City,kocha Guardiola amewatoa hofu wadau hao na mipango yake kwa msimu wa 2023/24.
Wengi wanaamini Nunez ni mchezaji anayekuwa mbadala wa Gundogan aliyeondoka klabu hapo na kujiunga na Barcleona lakini pia majeraha ya muda mrefu yatakayomweka Kelvin de Bruyne nje kwa muda mrefu basi nyota huyo ataokoa jahazi la timu hiyo .
Kwa upande wa Guardiola amenukuliwa akisema
" Matheus Nunez ni moja ya wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa.Mbali na kufanya makosa madogo madogo lakini nimeridhishwa kwa sababu tumechukua hatua mpya kuelekea hatua zinazofuata ,Nunez ni mchezaji bora kwa sasa"
0 Comments