BETI NASI UTAJIRIKE

BARCELONA WANAKWAMA WAPI NYAKATI HIZI

 Kama utakuwa mfuatiliaji wa La Liga hususani klabu ya Barcelona utagundua kuna mambo yanaendelea nyuma ya pazia na yanaacha maswali kwa wadau wa soka hasa mashabiki wa klabu hiyo.

Swali la kwanza ni kwanini klabu hiyo imeruhusu nyota wake Osman Dembele kutimkia PSG na kumtoa Kwa mkopo kinda wake Ansu Fati.

Nimejaribu kumfuatilia Ansu Fati tangu anasajiliwa na Barcelona,mpaka sasa amecheza mechi 100 tena kwa mafanikio makubwa kila alipopata nafasi ya kuanza chini ya kocha Xavi.

Msimu wa 2022/23 ulikuwa ni mzuri kwa upande wake hasa ukiangalia ni kijana mwenye miaka 20 tu lakini namba zake hapa chini si haba 


Kwa sasa nyota huyo amejiunga na Brighton inayoshiriki michuano ya Europa na ligi kuu ya Uingereza na thaman ya uhamisho huu wa mkopo ni dau la paundi milioni 7 sawa na kulipwa kiasi cha paundi 160,000 kwa wiki akiitumikia klabu hiyo .

Kuondoka kwa Ansu Fati nyakati hizi kunatafsiriwa kama kupunguza gharama za uendeshaji kwa klabu ya Barcelona. Utakumbuka Barcelona wameanza maboresho ya uwanja wao wa nou camp na mabilioni ya fedha yamekwishawekwa kukamilisha mpango kazi huo.

Kwa tafsiri nyepesi ni kuwa Barcelona wameamua kupunguza matumizi kwa kutonunua wachezaji wa gharama na kusajili nyota waliomaliza mikataba yao akiwemo Roberto Lewandowski na iker Gundogan ili kukamilisha maboresho hayo

Laporte amekuja na mkakati huu ili kukamilisha miradi ya viwanja na hata kuuzwa kwa Dembele ni mkakati wa kuongeza mapato ndani ya klabu hiyo.

Thamani ya real Madrid na Barcelona hazijatofautiana sana na hata project za maboresho ya viwanja vyao ni kama walijipanga,Mbali na Real Madrid kuwa na project za Santiago bernabeu lakini wamefanikiwa kunasa nyota wakubwa tena kwa gharama kubwa mno ukiwemo usajili wa Jude Bellingham kutoka Borrusia Dortmund swali la msingi hapa ni je Barcelona ya Laporte imekwama wapi kwa kuanza kutoa kwa mkopo wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Ansu Fati?

Kwangu Ansufati ni kama rodrigo, camavinga,vinicious jr na valvede kwamba ni wachezaji wa kikosi cha kwanza kwann klabu iwatoe kwa mkopo?

Kuna mahali Barcelona wanakwama 

 


 

Post a Comment

0 Comments