Mabingwa watetezi wa ligi kuu NBC klabu ya Yanga imefanikiwa kuwatoa kileleni Simba SC. Yanga walivuna pointi moja kutoka kwa Azam mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 na kuwafanya wafikishe pointi 7 kwenye michezo 3 huku wapinzani wao Simba wakiwa na pointi 6 na mchezo mkononi dhidi ya KMC mchezo utakaopigwa kesho saa 1:00 jioni.
Mchezo dhidi ya Azam ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili.Azam walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Daniel Amoah aliyefunga bao dakika ya 25 kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko Azam FC wakiongoza.
Kipindi cha pili Yanga walikuja kivingine baada ya kuwatoa Denis Nkane na Dickson Job kisha kuwaingiza Feisal Salum na Djuma Shaban. Dakika ya 57 Feisal Salum alipiga shuti nje ya lango la Azam na kufanikiwa kusawazisha bao hilo.
Dakika ya 65 Malik Ndoye wa Azam FC alifanikiwa kuwapa tena uongozi azam baada ya kumalizia pasi ya Abdul Sopu na kufanya Azam kuwa na mabao mawili. Dakika ya 77 ni Feisal Salum nje ya lango la Azam fc akafanikiwa kupiga suti kali lililozalisha bao la 2 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 2-2.
Kwa matokeo hayo Azam anasalia nafasi ya 4 akiwa na pointi 5 kwenye mech 3 alizocheza na yanga amepanda mpaka nafasi ya kwanza akiwa na pointi 7 kwenye mechi 3 walizocheza.
0 Comments