Mabingwa watetezi wa COSAFA Twiga Stars wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Botswana katika mchezo wa Kundi D michuano ya Wanawake ya COSAFA leo Uwanja wa Madibaz mjini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini.
Twiga Stars inafikisha pointi nne baada ya ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Comoro. Kwa pointi hizo Twiga Stars inajihakikishia nafasi ya kusonga hatua ya nusu fainali kama watashinda mchezo wao wa mwisho.
0 Comments