advertise with us

ADVERTISE HERE

TOMAS TUCHEL KWISHA HABARI YAKE CHELSEA

 Klabu ya Chelsea imetangaza rasmi kuachana na kocha wake mkuu Tomas Tuchel . Tuchel alijiunga na Chelsea mwaka 2021 akiwa kocha huru baada ya kumaliza mkataba wake na PSG. Tangu ajiunge na Chelsea amefanikiwa kuiongoza klabu hiyo katika mechi 100 akishinda mechi 60 ,sare mechi 24 na kufungwa mechi 16.


Akiwa kocha mkuu wa chelsea alifanikiwa kutwaa makombe kadhaa ikiwemo UEFA Champions League kwa msimu wa 2020/21 UEFA Super Cup 2021,Fifa Club world cup 2021. Msimu wa 2022/23 umeanza vibaya kwa Tomas Tuchel baada ya kutumia kiasi cha paundi milioni 286 kusajili nyota kama Cucurela,Aubemayang,Fofana,Koulibal na  Raheem Sterling lakini timu hiyo imeambulia vipigo vitatu dhidi ya Leeds United 3-0, Suthhampton 2-1 na mchezo wa Uefa dhidi ya Dinamo bao 1-0 . 

Mpaka sasa Chelsea wanashika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na point 10 kwenye mechi 6 walizocheza wakipata ushindi kwenye mechi 3 sare 1 na kufungwa mechi 2 

Uongozi wa Chelsea chini ya mmiliki mpya Todd umeshindwa kumvumilia Tuchel na wameamua kumvunjia mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili. 

Post a Comment

0 Comments