Chama cha soka nchini TFF kimejibu malalamiko ya klabu ya Yanga baada ya kumzuia Tuisila Kisinda kujiunga na miamba hiyo ya soka nchini.Yanga walimsajili kisinda kwa mkopo.akitokea RS BERKANE na ilidhaniwa mchezaji huyo angejumuishwa ndani ya timu hiyo kushiriki michuano NBC pamoja na Azam Sports Federation Cup.
Kwa mujibu wa TFF ni kuwa usajili wa Kisinda hautambuliki kwani klabu ya Yanga ilikwishakamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni na majina yao yalikwishawasilishwa CAF na leseni za wachezaji wa kigeni zilikwishatoka hivyo jina la kisinda halimo kwenye orodha hiyo
Hii hapa ni barua ikitoa ufafanuzi
0 Comments