Chama cha soka nchini TFF kimetoa majina ya wachezaji 25 wa klabu ya Yanga watakaotumika kwa msimu wa 2022/23 kwa ligi za NBC,Azam Federation Cup na michuano ya CAFCC. TFF wamesema jina la straika Crisipin Ngushi halikusajiliwa kwenye mfumo wa TFF wala CAF hivyo mchezaji huyo hatoweza kucheza kwa msimu huu.
Ngushi alijiunga na Yanga mwezi disemba 2021 akitokea Mbeya Kwanza lakini hakupata nafasi ya kucheza mechi nyingi. nyingi za kuanza ndani ya klabu hiyo.Bado haijawekwa wazi kama Yanga watamtumia mchezaji huyo kwa msimu huu . Haya hapa ni majina ya wachezaji watakaocheza kwa msimu huu.
0 Comments