ads

adds

SEHEMU YA KWANZA: SABABU ZA LEICESTER CITY KUKWAMA MSIMU HUU

 Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa EPL basi utakuwa unajiuliza ni nini hasa kimetokea kwa klabu ya Leicester City mpaka kucheza mechi 6 na kupata pointi 1 tu wakikaa nafasi ya 20 kwenye msimamo wa ligi kwa msimu wa 2021/22.


Historia fupi kwa Leicester City 

Klabu hii ilipanda ligi kuu Uingereza mwaka 2014 na msimu huo  ilifanikiwa kwa kumaliza nafasi ya 14. msimu wa 2015/16 iliushangaza ulimwengu wa soka baada ya kuibuka mabingwa wapya wa EPL wakifikisha pointi 81 kwenye mechi 38 walizocheza na nafasi ya pili ikichukuliwa na Arsenal waliojikusanyia pointi 71 kwa mechi hizo hivyo kupishana kwa pointi 10. 

Mbali na kutwaa Ubingwa wachezaji mbalimbali wa Leicester City walitwaa tuzo mbalimbali zikiwemo za mchezaji bora iliyokwenda kwa Riyad Mahrez,Mfungaji Bora alikuwa ni Jamie Vardy akifunga mabao 24 ,Kocha bora akiibuka ni Claudio Ranieri .Mchezaji ora kwa waandishi wa habari aliibuka Jamie Vardy.

Tuzo ya kikosi bora cha mwaka Leicester walifanikiwa kuwaingiza wachezaji watatu akiwemo Beki Wes Morgan kiungo Ng'olo Kante na Mshambuliaji akiwa ni Jamie Vardy

Msimu wa 2016/17

Msimu huo haukuwa mzuri kwa Leicester City baada ya kumaliza nafasi ya 12 ,kuondoshwa raundi ya tatu kwenye michuano ya EFL na FA CUP. Ngolo Kante aliuzwa na klabu hiyo kwa dau la paundi milioni 32 kwenda Chelsea.

Msimu wa 2017/18

Msimu wa 2017/18 walirejea kwa kasi baada ya kufika Robo fainali kwenye michuano ya EFL na FA huku wakishika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi.Walimuuza kiungo wao mahili Dany Drinkwater kwa paundi milioni 35 kwenda Chelsea na kumnunua Ihenacho kwa paundi milioni 25 kutoka Manchester City huku ikiwaacha wachezaji 7.

Msimu wa 2018/19 

Leicester walimuuza Riyad Mahrez kwenda Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 huku ikiwaacha wachezaji wengine 10. Msimu huo hautasahaulika kwa mashabiki wa Leicester City. 

Ni tarehe 27 Oktoba 2018 mara baada ya mchezo dhidi ya Westham mmiliki wa klabu hiyo Bwana Vichai Srivaddhanaprabha Pamoja na abiria wengine wanne walipanda helikopta yao iliyofika uwanjani hapo kuwachukua  na baada ya dakika kadhaa hewani ilianguka na watu wote kupoteza maisha .

Tangu kutokea kwa Ajali hiyo timu hiyo iliyumba kiuchumi na kiutendaji huku ikizidi kufanya vibaya kwenye mechi zake hivi karibuni.

Msimu wa 2022/23 

Leicester wamecheza michezo 6 mpaka sasa wakipata sare mchezo mmoja na mingine 5 wakifungwa. Walipata sare mchezo wa kwanza dhidi ya Brentford ya mabao 2-2.  Walifungwa na Arsenal 4-2.Walifungwa 2-1 na Southampton,walifungwa 2-1 na Chelsea. Walifungwa 1-0 na Manchester City .Wamefungwa 5-2 na Brighton.

USAJILI 

kwa msimu huu Leicester wamesajili wachezaji wawili tu ambao ni golikipa Alex Smithis na beki Wout Faes. 

Swali ni je nini hasa kimeikumba Leicester City? Endelea kufuatilia sehemu inayofuata.

Post a Comment

0 Comments