advertise with us

ADVERTISE HERE

MWAKINYO ATOA SABABU ZA KUPIGWA NA LIAM SMITH

 Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amepoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith ,pambano lililopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Liverpool nchini Uingereza.Pambano hilo lenye Raundi 12 lilimalizika raundi ya tatu baada ya  Mwakinyo kuonekana amepata majeraha ya mguu.


Katika Pambano hilo Mwakinyo alitawala raundi zote tatu za mwanzo lakini refarii aliamulu pambano hilo kuweza kumalizika baada ya Mwakinyo kutema Mouth Guard mara mbili kwa kushindwa kuvumilia maumivu ya mguu aliyoyapata ulingoni. Mara baada ya pambano Mwakinyo amefunguka na kusema 

"Mambo vipi watanzania,Asanteni sana kwa sapoti yenu mnayonipa. Mechi kama mlivyoiona begi langu lilipotea Airport wakati nakuja huku kwahiyo jamaa imebidi wanipe viatu vingine vipya ko wakati napigana viatu vyao vilikuwa vinanifinya sana kama nimepata enka ndio maana nikatema mouth guard chini kwa sababu sheria ya boxing inasema ukitema mouth guard chini maana yake refarii anatakiwa aiokote mouth guard amsimamishe mpinzani aniulize kunaendelea nini, ko nilimuambia nina enka akaniuliza naweza kuendelea nikamwambia naweza"

"baada ya kuendelea ile Enka imenishika tena nimeshuka yule mpinzani wangu akaniongezea ngumi pale pambano limeisha kwa TKO lakini mimi sihesabu kama ni TKO kwa sababu nyie wenyewe mmeona .Nashukuru sana lakini tunajaribu kuongea na promota niwekewe rematch naye kwa sababu naamini ninauwezo wa kufanya kitu.Nawapenda sana Mashabiki zangu"Post a Comment

0 Comments