MSHAHARA WA MAYELE NI KUFURU NDANI YA YANGA

 Fiston Kalala Mayele anaendelea kubakia ndani ya Yanga kwa msimu wa 2022/23 na 2023/24. Mayele alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2021/22 kwa mkataba wa mwaka mmoja. Taarifa za ndani zinasema Mayele alikataa kusaini mkataba mpya na Yanga kwa sababu za kimasilahi lakini uongozi wa Yanga ukaamua kumpa kile alichotaka na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Inasemekana mkataba huu mpya kwa Mayele utamfanya awe ni mchezaji anayelipwa zaidi Yanga na ligi kuu NBC. Mayele anaungana na wachezaji wengine wa Yanga kama  Farid Musa ,Djuma Shabani ,Yanick Bangala na Zawadi Mauya walioongeza mikataba yao mpaka mwaka 2024.

Kwa msimu uliomalizika Mayele alishika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi ya NBC akiwa na mabao 16 nyuma ya George Mpole wa Geita Gold aliyekuwa na mabao 17. Kubwa zaidi ni mchezaji huyo kuwafunga Simba mabao matatu kwenye michezo mitano waliyokutana kwa msimu wa 2021/22.

Mayele kusalia ndani ya Yanga kutaifanya safu ya ushambuliaji kwa Yanga kuwa na kikosi imara kuelekea michezo dhidi ya AZAM na Zalan FC 

Post a Comment

0 Comments