Pambano hilo litapigwa Septemba 30 katika Hotel ya Next Door Arena na linategemewa kuwa na watazamaji wengi huku pia makampuni ya kurusha tangazo hilo mbashara yakikaribishwa kudhamini pambano hilo kubwa na la kwanza kwa kampuni ya MOBOXING
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Mohammed Dewji zinasema tajiri huyo amedhamilia kuwekeza pesa nyingi kwa mchezo wa masumbwi na kubadilisha maisha ya vijana wanaoutumikia mchezo huo. Kuwekeza ndani ya boxing kutawafanya watanzania wengi wanufaike na kupunguza tatizo la ajira nchini.Mohammed Dewji ambaye pia mmiliki wa hisa 49% ndani ya Simba amekuwa msaada mkubwa kwa vijana akiwapa ajira kupitia viwanda vyake na fursa ya kusomeshwa kwa wanafunzi wasiojiweza kiuchumi kupitia taasisi ya MO DEWJI FOUNDATION.
Uongozi wa AMOSPOTI HOLDINGS TANZANIA LTD kupitia mkurugenzi wake Bw.Amos Medeck upo tayari kuungana na MoBoxing kulitangaza pambano hili mubashara kupitia mitandao ya kijamii
0694021861
0 Comments