MANCHESTER UNITED BABA LAO YAISAMBARATISHA ARSENAL BILA YA HURUMA

 Manchester United imeendeleza ubabe wake EPL baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Arsenal mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford.Magoli ya Manchester United yaliwekwa kimiani na Antony Dos Santos aliyefunga bao la kwanza dakika ya 35 akipokea pasi kutoka kwa Marcos Rashford. 


Mabao mengine yalifungwa na Rashford akipokea pasi kutoka kwa Bruno Fernandez dakika ya 66 na bao la tatu akipokea pasi kutoka kwa Christen Eriksen dakika ya 66

Rashford aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo kwa kufunga mabao mawili na assist 1. Bao pekee la Arsenal lilifungwa na Saka dakika ya 60 kwenye  mchezo huo. 

Kabla ya mchezo huo Arsenal ilikuwa imecheza mechi 5 na zote kupata ushindi wakijikusanyia pointi 15 na kubakia kileleni mwa msimamo wa ligi.. 

Manchester United chini ya kocha Erik ten Hag imecheza kwa kiwango cha hali ya juu kwa mechi ya nne mfululizo na kuifanya timu hiyo kujikusanyia pointi 12 katika mechi 6 walizocheza. 

Post a Comment

0 Comments