BETI NASI UTAJIRIKE

LIVERPOOL HALI MBAYA ,CHILWELL NA HAVERT WAIBEBA CHELSEA

 Michezo ya ligi kuu Uingereza imeendelea wilkiendi hii kwa kuzikutanisha timu mbalimbali. Mechi iliyozua gumzo ni mchezo kati ya Brentford dhidi ya Leeds United mchezo uliomalizika kwa Brentford kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.

Liverpool vs Everton

Mechi nyingine iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ni Liverpool dhidi ya Everton mchezo uliuomalizika kwa timu hizo kutoa sare ya bila kufungana na kuifanya Liverpool kufikisha pointi 9 tu katika mechi 6 alizocheza msimu huu wakiwa nafasi ya 6. Liverpool iliendelea kuwaamini wachezaji wake wa kikosi cha kwanza wakianza na Allison kwa Golini mabeki wakiwa ni Arnold,Tsmikas,Joe Gomez,Van Dijk, na Viungo tegemez Fabinho,Fabio na Elliot huku eneo la ushambuliaji wakianza na Mo Salah,Nunez na Luis Diaz.

Chelsea vs Westham United 

Chelsea wameendeleza ubabe kwa mechi ya 3 mfululizo baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Westham United. Chelsea walitawala nyakati zote za mchezo lakini mabeki wa Westham walikuwa imara na kuwafanya Pulisic na Sterling washindwe kupenyeza ngome yao. Kipindi cha pili kocha Tomas Tuchel alifanya mabadiliko dakika ya 72  kwa kumtoa Cucurela na nafasi yake kuchukuliwa na Chilwell aliyefunga bao dakika ya 76 akipokea pasi kutoka kwa Thiago Silva huku  Kovavic na nafasi yake ikichukuliwa na Kai Havert  aliyefunga bao la pili dakika ya 88 akipewa pasi na Chilwell.

Kwa matokeo hayo Chelsea anakuwa na point 10 kwenye mechi 6 alizocheza akiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.


Post a Comment

0 Comments