advertise with us

ADVERTISE HERE

HIZI HAPA MECHI ZITAKAZOMUONDOA ZORAN MAKI SIMBA

 Kocha mkuu wa Simba Zhoran Maki anakibarua kigumu mno kwa mwezi Septemba. Kibarua hicho ni kuhakikisha anapata ushindi kwenye mechi 6 atakazocheza ndani ya siku 23 tu swali ni je kwa ratiba hii Zoran Maki abaki Simba au safari itakuwa imewadia

Tarehe 03 Septemba Simba itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arta Solar ya nchini Djibouti timu iliyosheheni wachezaji waliowahi kuvichezea vilabu vya Arsenal na Barcelona ambaye ni Alexander Song na Solomon Kalou aliyecheza Chelsea.

Tarehe 7 watacheza mchezo wa ligi kuu NBC dhidi ya KMC mchezo utakaopigwa dimba la Benjamini Mkapa,Tarehe 10 timu hiyo itacheza mchezo wa Raundi ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullet nchini Malawi na itarejea nchini kucheza mchezo mgumu dhidi ya Tanzania Prisons dimba la Sokoine Mbeya  tarehe 14 kisha kurudiana na Nyasa Big Bullet dimba la Benjamini Mkapa tarehe 17.

Tarehe 28 timu hiyo itacheza mchezo wa ligi kuu NBC dhidi ya Mbeya City dimba la Sokoine Mbeya. Simba wanakibarua kigumu mno kuhakikisha wanapata ushindi wa mechi zote tano za kimashindano na kama watapoteza mchezo wowote hasa dhidi ya Nyasa Big Bullet basi Kocha Zoran Maki atakuwa na maisha mafupi ndani ya Simba. 

Hii hapa ratiba ya Simba kwa Mwezi Septemba 

Ikumbukwe Kocha huyo alikubaliana na Simba kuhakikisha timu hiyo inafika nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika na inarejesha makombe ya NBC pamoja na Azam Sports Federation Cup na kama atashindwa moja kati ya hayo ataondoshwa klabuni hapo.

Post a Comment

0 Comments