BETI NASI UTAJIRIKE

HALAAND AWEKA REKODI MPYA AKIWAPOTEZA BENZEMA,NEYMAR ,LEWANDOWSKI NA MBAPPE

 Erling Halaand ameendelea kugonga vichwa vya habari duniani kote kwa uwezo mkubwa wa kufunga mabao. Wiki iliyopita nyota huyo aliandika historia kwa kufunga Hat Trick mbili mfululizo dhidi ya Nottingham Forest na Crystal palace na kumfanya afikishe mabao 10 kwenye mechi 6 alizokwisha cheza.

Rekodi ya kipekee kwa Halaand ni kufunga hat trick zote mbili kwa dakika 45 . Mchezo dhidi ya Nottingham Forest alifunga mabao dakika ya 12,23 na 38 kipindi cha kwanza huku mchezo dhidi ya Crystal Palace akifunga mabao dakika ya 62,70 na 81.Kinachoshangaza zaidi ni kuona Halaand anafunga kwa michezo minne mfululizo na kumfanya awe na mabao 10 mengi zaidi kwa wachezaji wote wanaoshiriki ligi mbalimbali ulaya.

Mbappe na Neymar wamefunga mabao 7 kila mmoja katika mechi 6 walizocheza Ligue 1 pale ufaransa, Kwa upande wa La Liga Roberto Lewandowski ana mabao 5 huku Benzema  akiwa na mabao 3.

Kwa Bundesliga Sheraldo Becker anamabao matano katika mechi 5 alizocheza. Kama Halaand ataendelea kwa spidi hii basi atajiwekea mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha mfungaji bora Ulaya kwa mwaka 2022/23


Post a Comment

0 Comments