BETI NASI UTAJIRIKE

HAKUNA WA KUMUONDOA ARSENAL KILELENI

 Klabu ya Arsenal imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ya Uingereza maarufu kama EPL baada ya mpinzani wake wa karibu Manchester City kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Aston Villa. Sare hiyo inawafanya Manchester City kusalia nafasi ya 2 wakiwa na pointi 14 baada ya michezo 6.

Arsenal inaongoza msimamo wa ligi na leo hii itavaana na Manchester United kwa mchezo wa raundi ya 6. Kwa sasa Arsenal wanapointi 15 kwa michezo 5 waliyokwisha cheza na hakuna timu yoyote inayoweza kufikia pointi hizo kwa raundi 6 walizocheza.

Kwa upande wa Tottenham Hotspurs  wao wanapointi 14 na wamekwisha cheza michezo 6 ,kama itatokea Arsenal akafungwa mchezo dhidi ya Manchester United basi atasalia kileleni akiwa na pointi 15 na kama atashinda basi atakuwa na pointi 18 hivyo kuwazidi Manchester City na Tottenham kwa pointi 4.

Huu ni mwanzo mzuri kwa Arsenal na kama timu hii itaendelea kucheza kwa kiwango hicho tutegemee kuona timu hiyo ikifanya makubwa zaidi kwenye michuano mbalimbali ikiwamo Europa League ,Carabao Cup,FA Cup na EPL

Post a Comment

0 Comments