Azam wamefanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chao kwa kuwasajili wachezaji wa kimataifa na wenye umri mdogo huku pia wakiimalisha benchi la ufundi kwa kuwaleta madaktari,makocha wa viungo,washambuliaji ,makipa na sasa wamemuongeza Denis Lavagne kama kocha mkuu.
Kocha Denis Lavagne amekwishawahi kuwa mchezaji wa timu mbalimbali za ufaransa tangu mwaka 1981 akicheza nafasi ya ulinzi na baada ya kustaafu alijiunga na kozi za ukocha mwaka 1989. Hizi ni timu ambazo Denis Lavagne amekwishazichezea mpaka sasa.
Apps | (Gls) | ||
1981–1982 | Le Havre B | ||
---|---|---|---|
1982–1983 | Rouen B | ||
1983–1984 | Béziers | ||
1984–1985 | Alès | ||
1985–1987 | Orange | ||
1987–1989 | Alès B |
Kocha huyu mkuu anauzoefu na soka la Africa na pia anamiliki leseni kubwa ya UEFA Pro Licence.Rekodi zake zinaonyesha ameanza kufundisha soka mwaka 1998 na amefundisha jumla ya vilabu 14 na Azam itakuwa ni timu ya 15. mwaka 1998-99 alifundisha Deveze na Baadaye alijifundisha timu zifuatazo
1999–2003 | Sedan B | ||
---|---|---|---|
2007–2008 | Coton Sport | ||
2009–2011 | Coton Sport | ||
2011–2012 | Cameroon | ||
2013 | Étoile du Sahel | ||
2013–2014 | Al Ittihad Alexandria | ||
2014 | Najran | ||
2014–2015 | Smouha | ||
2015–2016 | MAS Fez | ||
2016 | Free State Stars | ||
2016–2017 | Al-Hilal | ||
2018–2019 | CS Constantine | ||
2021 | JS Kabylie | ||
2021 | USM Alger |
0 Comments