Uongozi wa Azam Complex umevipa changamoto vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara na timu za nje ya nchi kwa kuhakikisha wanatoa pesa kama watataka kutumia uwanja wao kwa mazoezi au mechi mbalimbali.
Uongozi wa Azam Complex umefikia hatua hiyo baada ya marekebisho makubwa waliyoyafanya mwishoni mwa msimu huu kwa kuweka Nyasi Mpya Bandia ,Mabango ya matangazo na Taa kwa ajili ya mechi za usiku. Tangazo hilo limevilenga vilabu vya Simba na Yanga ambavyo mpaka sasa vinatimiza miaka 86 na 87 lakini havina viwanja vya mechi huku vikitegemea uwanja wa Benjamini mkapa.
Katika tangazo lilotoka hivi karibuni limeonekana kuhitaji pesa endapo timu yoyote itataka kutumia uwanja wao. Timu nyingine kama KMC na Ruvu Shooting za mikoa ya Dar es salaam na Pwani zitalazimika kuomba mechi zake za nyumbani ziwe katika viwanja vya Benjamini Mkapa na Uhuru.
Mpaka sasa vilabu vinavyomiliki na kutumia viwanja vyenye nyasi bandia ni Azam FC- AZAM COMPLEX, Kagera Sugar ,Wakati vilabu kama Namungo- wao wamekwishatandika nyasi bandia kwenye uwanja wa Majaliwa Stadium na Geita Gold wanakamilisha ujenzi wa uwanja wao
0 Comments