ANAYEMWAGA FEDHA SIMBA QUEENS ATAJWA .BASI JIPYA BABA LAO

 Klabu ya Simba Queens imeanza kuneemeka kuelekea msimu mpya wa 2022/23  baada ya leo hii kukabidhiwa basi jipya la kisasa kutoka kampuni ya African Carriers. Kampuni hii iliingia mkataba na klabu ya Simba kwa ajili ya udhamini wa mabasi matatu ambapo mwaka 2021 iliwakabidhi Simba basi la Kisasa kwa ajili ya timu ya wanaume .

Leo wamekabidhi basi la pili kwa ajili ya Simba Queens na wanategemewa kukabidhi basi la tatu kwa ajili ya timu ya Vijana. Uongozi wa Simba chini ya Barbara Gonzalez umezidi kuneemeka siku hadi siku kwa mikataba minono ambayo klabu hiyo imekuwa ikiingia.

Mwezi July klabu ya Simba iliingia mkataba mnono wa bilion 26 na kampuni ya M-BET kwa udhamini wa miaka mitano na mkataba huo hauzihusishi timu za vijana wala Simba Queens. Kwa  sasa wanamtafuta mdhamini mkuu kwa upande wa Simba Queens na timu ya vijana.
Barbara amenukuliwa akisema 

"Zamani Simba Queens ilikuwa inatumia Coaster kwa safari za ndani lakini kwa sasa wamepata basi kubwa na zuri,ukiona mdhamini mkubwa kama hivi anajitolea basi ujue ameona matunda ya Simba Queen na thamani ya Klabu kwa ujumla. Kabla ya ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake haijaanza tutakuwa tumepata mdhamini mkuu na tutamtangaza."

"Mafanikio haya yote mnayoyaona ni uwekezaji wa Mohammed Dewji ndani ya Simba"

Post a Comment

0 Comments