advertise with us

ADVERTISE HERE

HATMA YA YACOUBA NDANI YA YANGA YAWEKWA WAZI

 Winga Yacouba Sogne anaweza kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa msimu wa 2022/23. Mpaka sasa klabu ya Yanga inajumla ya wachezaji 13 wa kigeni na majina ya wachezaji 12 yamekwishawasilishwa bodi ya ligi huku jina la Yacouba Sogne likikosekana na kumfanya nyota huyo kutakiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa pekee.


Awali kulikuwa na uvumi kuwa nyota huyo ataondoka mwishoni mwa msimu wa 2021/22 baada ya mkataba wake na klabu hiyo kumalizika lakini mpaka sasa nyota huyo ameendelea kufanya mazoezi na timu hiyo iliyo kambini Avic Town. Sheria za CAF zinaruhusu timu moja kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa kugeni na wazawa hiyo itampa nafasi Yacouba Sogne kucheza mechi za kimataifa.

Yacouba atatakiwa amshawishi kocha Nabi ili aweze kujihakikishia namba kwa kikosi kitakachoshiriki Champions League kwa raundi ya kwanza na Zalam FC ya nchini Sudan Kusini.Itakumbukwa Yacouba aliumua katikati ya msimu uliomalizika na YAnga waliahidi kumhudumia mpaka atakaporejea uwanjani ,uwepo wake ndani ya Yanga kwa sasa ni ishara kwamba klabu hiyo inahitaji huduma yake.

Post a Comment

0 Comments