Klabu ya Geita Gold im,eendelea kujiimarisha kuelekea msimu wa 2022/23 baada ya kunasa saini ya beki wa kulia aliyekuwa anaichezea Dodoma Jiji Aman George Wawa . Awali klabu hiyo ilikuwa kimya tangu kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili na sasa wameanza kuweka hadharani siraha watakazotumia kwa msimu wa ujao hasa kimataifa na ligi kuu.
Ikumbukwe Geita Gold itashiriki Kombe la Shirikisho baada ya kumaliza ligi wakiwa nafasi ya Nne nyuma ya Azam FC. Wawa anakwenda kugombea namba na beki wa timu hiyo David Kameta na anategemewa kuleta ushindani mkali. lakini kuondoka kwa Juma Nyoso kutamfanya David Kameta kurejea eneo la beki wa kati kama alivyokuwa akicheza Coastal Union kabla ya kutua Simba na Baadaye geita na kama atawekwa nafasi hiyo na kocha Fredrick minziro maana yake Kelvin Yondani atatengeneza ushirikiano na Duchu huku Adeyun Salehe na Wawa wakicheza pembeni
Mchezaji huyo aliwahi kuitumikia Singida United na baadaye Dodoma jiji alitambulishwa hadharani leo mchana na amesaiini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu yake hiyo mpya.kupitia mitandao ya kijamii Geita Gold waliandika
" Geita Gold tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba na mlinzi wa kulia George Aman Wawa "
"George Aman Wawa alikuwa akiitumikia klabu ya Dodoma Jiji ,Moja kati ya mafundi wa mpira wenye akili ya ulinzi na mbinu za kisasa.Karibu Geita ,Karibu saana kwa wawakilishi wa kimataifa"
0 Comments