PROFESA NABI NA REKODI ZAKE NDANI YA YANGA NA TANZANIA

 Hatimaye kocha mkuu wa klabu ya Yanga Nasredinne Nabbi amekabidhiwa tuzo yake kama kocha bora kwa msimu wa 2021/22. Nabi aliyewasili mwanzoni mwa msimu huo aliweka rekodi ya kipekee baada ya kucheza mechi 30 za ligi ya NBC pasipo kufungwa mechi hata moja (Un Beaten) na kumfanya aingie kwenye vitabu vya rekodi ndani ya Tanzania na klabu ya Yanga


Nabi aliiongoza Yanga kutwaa ubingwa wake wa 28 wa ligi kuu kwa kucheza mechi 30 na akashinda mechi 22 huku akipata sare 8 na kufunga jumla ya mabao 49 na akifungwa mabao 8 tu . Rekodi hii ilimfanya Nabi kuondoka na tuzo ya Kocha Bora wa msimu wa 2021/22 kwa NBC PREMIER LEAGUE na kuwa kocha mwenye Rekodi ya aina yake kwa msimu huo.

itakumbukwa ni vilabu vitatu tu ndivyo vilitwaa ubingwa wa ligi kuu pasipo kufungwa tangu kuanza kwa ligi yetu pendwa .Simba msimu wa 2011/12, Azam FC 2013/14 na Yanga 2021/22

Kocha Nabi aliisaidia Klabu ya Yanga kutwaa kombe la Ngao ya Jamii mwanzoni mwa msimu na kutwaa kombe la Azam Federation na kuifanya Yanga itembee kifua Mbele kwa Msimu huo.Kocha Nabi ataendelea kuwepo ndani ya Klabu ya Yanga kwa msimu wa 2022/23 na ataongoza miamba hiyo kuelekea michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE,NBC PREMIER LEAGUE NA ASFC

Post a Comment

0 Comments