Klabu ya Manchester imemtambulisha nyota wake mpya Christian Eriksen. Nyota huyu aliyesajiliwa kama mchezaji huru anategemewa kufanya makubwa kwa msimu huu hasa eneo la kiungo kutokana na rekodi nzuri alizojiwekea akitumikia vilabu mbali mbali vya ligi ya Uingereza.
Eriksen amecheza jumla ya michezo 237 akiwa na Tottenham msimu wa 2013/14 na baadaye Brentford .Akiwa na vilabu hivyo alifanikiwa kufunga mabao 52 akitengeneza mabao 66 na kumfanya awe ni moja ya wachezaji wenye mafanikio ndani ya EPL
Manchester United inaamini uwepo wa Nyota huyo utaleta matokeo chanya ndani ya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2022/23 na wanaamini atakwenda kuziba nafasi zilizoachwa na Paul Pogba na Nemanja Matic waliotimkia vilabu vya Italy Juvenus na As Roma.
0 Comments