AHMED ALLY ATAMBA SIMBA IKIWEKA REKODI MPYA LEO

 Klabu ya Simba imeendelea kufanya vizuri  nje ya uwanja kwa mwezi julai na hii ni baada ya kufanikiwa kuwafikia watumiaji wake wa mitandao ya kijamii ikiwamo Twitter ,Youtube achilia mbali Facebook na Instagram.


Kupitia taarifa kamili iliyotolewa na klabu hiyo ni kuwa leo hii imefanikiwa kupata wafuatiliaji milioni 1 katika mtandao wa Twitter ,wafuasi laki 3 katika mtandao wa Youtube, wafuasi milioni 1 katika mtandao wa Facebook na wafuasi milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram.Kwa namba hizo klabu ya Simba imewazidi wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga kwenye kila eneo la mtandao wa kijamii kwani wao wanawafuasi milioni 1.9 Instagram ,wafuasi laki 5.64 facebook .Wafuasi laki 1.84 Youtube.

Taarifa hii inaifanya klabu ya Simba kuongoza kwa kufuatiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwa nchi za Afrika Mashariki lakini pia ni klabu iliyowahi kuongoza kwa kufuatiliwa Afrika msimu wa 2020/21 baada ya kuzifunga klabu za As Vita ,Mamelidi,Al Ahly Keizer Chiefu ,Al Merreikh na vilabu vingine vikubwa Africa

Idara ya Habari ya Simba inayoongozwa na Ahmed Ally imeipiku Idara ya Habari ya Yanga inayoongozwa na Hassan Bumbuli hivyo Yanga wanakazi ya ziada kuweza kuwapiku wapinzani wao klabu ya Simba.


Post a Comment

0 Comments