BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 20-06-2022

 Real Madrid tayari wanapanga kuanzisha kipengele cha kutolewa cha euro 150m (£128m) katika kandarasi ya mshambuliaji mpya wa Norway aliyenunuliwa na Manchester City Erling Haaland mnamo 2024. (AS)

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 27. (Fabrizio Romano, via Express)



Manchester United wana matumaini kwamba Barcelona watapunguza  bei yao ya £80m kumuuza kiungo waUholanzi wa miaka 25- Frenkie de Jong kwa £10-15m. (Athletic, usajali unahitajika)

Kocha wa United Erik ten Hag amewaambia wakuu wa klabu hiyo kumsajili De Jong na kiungo wa kati wa Uswidi Christian Eriksen, 30, kwani watakuwa sehemu muhimu ya timu yake. (Mirror)

Frenkie de Jong

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Frenkie de Jong

Mlinzi wa Manchester United Phil Jones, 30, yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaosakwa na Leeds United, lakini Whites huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Southampton na Fulham ambao pia wanamtaka  Muingereza huyo. (Marca - usalili . unahitajika)

Liverpool wanajiandaa kumpoteza mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 30, kwa uhamisho wa bure msimu ujao wa joto baada ya kukataa kutimiza matakwa ya mkataba wake wa pauni 400,000 kwa wiki. (Mirror)

Mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Sala

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Manchester City wako tayari kumruhusu mchezaji wa matumizi Oleksandr Zinchenko, 25, kuondoka katika klabu hiyo - huku Everton ikiripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine- City wakiandaa ofa ya kumnunua beki wa kushoto wa Brighton Mhispania Marc Cucurella, 23. (Fabrizio Romano).

Brighton wanatarajia kupokea takriban pauni milioni 50 kwa Cucurella, jambo ambalo linaweza kuwalazimu City kujitenga na mkataba huo. (Athletic, usajili unahitajika)

Oleksandr Zinchenko

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Liverpool wamemwambia mlinzi Neco Williams, 21, kwamba anaweza kwenda kwa mkopo msimu ujao, huku Nottingham Forest ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. (Mirror)

Ajax wamekataa dau la pauni milioni 25 kutoka kwa Arsenal kwa ajili ya kumnunua mlinzi wao wa kimataifa wa Argentina Lisandro Martinez, 24. (Mail)

Post a Comment

0 Comments