SADIO MANE HUYOO BAYERN MUNICH NJIA NYEUPE

 Klabu ya Bayern Munich imekaribia kuafikiana na Liverpool dau la paundi milioni  42.5 kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu hiyo Sadio Mane. Hapo awali miamba hiyo ya Ujerumani iliweka mezani dau la paundi milioni 30 ili waweze kumnasa nyota huyo lakini Liverpool walikataa ofa hiyo wakitaka nyongeza zaidi.


Bayern Munich wanaamini mchezaji huyo ni muhimu zaidi nyakati hizi ikizingatiwa wamekuwa na wakati mgumu baada ya nyota wake Robert Lewandowski kutangaza  kuondoka klabuni hapo baada ya kudumu miaka 10 na miamba hiyo.

Kwa msimu wa 2021/22 Mane amekuwa na kiwango bora na amepata mafanikio makubwa kwanza kwa kusaidia timu hiyo kubeba makombe ya Carabao Cup na FA huku akiwapeleka Senegal kombe la dunia nchini Qatar na kumaliza nafasi ya pili champion ligi na ligi kuu Uingereza.

Sadio Mane mwenyewe amekuwa akichochea suala la yeye kuondoka ndani ya Liverpool na chanzo kikubwa ni mapato anayopata ndani ya Liverpool.

Post a Comment

0 Comments