BETI NASI UTAJIRIKE

PAPE OSMAN SAKHO ATUMIA DAKIKA 13 KUISAMBARATISHA KMC

 Kiungo mshambuliaji wa Simba Pape Osman Sakho ameendelea kuwa mwiba mkali kwa kila anayokutana nayo msimu huu. Nyota huyu Msenegal ameendelea kuonyesha ubora wake kwenye mchezo mwingine wa ligi kuu NBC dhidi ya KMC baada ya kuiharibu Mbeya City wiki iliyopita.

Mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0 huku Sakho akifunga mabao mawili moja likiwa ni penati na jingine likiwa ni uwezo binafsi,nyota huyo ameendeleza ubora wake kwenye Mchezo dhidi ya KMC  baada ya kufunga bao 1 huku akitengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Kibu Denis na Inonga Baka mchezo uliomalizika kwa Simba 3-1 KMC.

Ilimchukua dakika 13 tu kwa Sakho kufanya maajabu hayo na kumfanya aibuke mchezaji bora wa mechi kwa mara ya pili mfululizo.Ikumbukwe nyota huyu aliweka rekodi ya kipekee kwenye michezo ya kombe la Shirikisho baada ya mabao yake mawili kuchaguliwa na kuwa mabao bora ya wiki.




Post a Comment

0 Comments