Klabu ya Manchester United imetangaza kuachana na Paul Pogba na Jesse Lingard mwishoni mwa msimu huu. Wachezaji hao wameondoka United baada ya mikataba yao kufikia kikomo.
Jesse Lingard amedumu kwenye kikosi cha Manchester United tangu akiwa na miaka 9 wakati pogba akiitumikia klabu hiyo kwa nyakati mbili tofauti
Kwanza akipandishwa kutoka timu ya vijana ya Man Utd na baadaye aliondoka klabuni hapo kuelekea Juventus ya Italy kisha baadaye kurejeshwa klabuni hapo kwa dau la Paundi Milioni 89 akiwa mchezaji aliyenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi na Manchester United. mwaka 2022 Pogba anaondoka klabuni hapo kama mchezaji huru na kuna uwezekano nyota huyo mwenye miaka 29 akaelekea Italy kuitumikia Juventus kwa mara nyingine.
Upande wa Manchester United
Klabu hiyo imeandaa dau la paundi milioni 72 kumshawishi nyota wa Barcelona Frenkie De Jong. Mchezaji huyo alijiunga na miamba hiyo ya soka ya Uhispania akitokea Ajax ya Uholanzi na kwa wakati huo alikuwa chini ya kocha mpya wa Man Utd Erik Ten Hag.
Manchester United wanaamini kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 25 kutaziba nafasi ya pogba aliyekwisha ondoka. Kwa upande mwingine Man utd wanaamini uwepo wa kocha Erik Ten Hag utamshawishi mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo ingawa mchezaji huyo anataka timu inayoshiriki michuano ya UEFA.
0 Comments