Matola anaamini anatosha kuwa kocha mkuu wa Simba lakini suala hiyo kwa sasa anawaachia mabosi wake ikizingatiwa kwamba nyota huyo wa zamani wa Simba ameitumikia Simba kwa miaka 5 mfululizo kama kocha msaidizi na baadaye kama kaimu kocha mkuu baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Franco Martinez kuondoshwa klabuni hapo kwa mwenendo mbaya.
Mara baada ya mchezo dhidi ya KMC kumalizika Matola alinukuliwa akisema
"Nashukuru kwa nafasi hii niliyopo sasa ,tunaenda kujipanga kwa ajili ya mechi zilizobaki ili uhakikisha tunashinda zote na kumaliza vizuri,
"Kuhusu msimu ujao kuna mambo bado hayajakamilika ,yapo kwenye uongozi na yakikamilika basi mtajulishwa nini kinafuata ila sasa muda bado na nasikilizia kila kitu kikikaa sawa"
0 Comments