BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA EDGAR KATEMBO:NAMNA BORA YA KUSHAMBULIA

 SHERIA NAMBA 10 YA SOCCER,  GOAL SCORING (namna goli linavyofungwa).........

       Goli litahesabika kuwa limefungwa ikiwa,

1.Mpira wote umevuka mstari wa goli(goal line).

 2.Hakuna faulo iliyofanyika kabla ya goli kufungwa.

 3. Mfungaji hskuwa kwenye nafasi ya kuotea/kuzidi/offside.

Naendelea kufatilia mahusiano kati ya sheria namba 10 na jezi namba 10( Maradona, Ronaldinho, Messi, )


        MEDDIE KAGERE na FISTON MAYELE........Hawa ni wachezaji ambao wanacheza katika nafasi ya  ushambuliaji.Wote wako physical, aggressive, wazuri miguu yote wazuri kichwani, hawahofii contact ardhini au hewani,wote wanaweza kufunga mbali na karibu.

      Pamoja na sifa zao hizo walizofanana pia wanafanana mapungufu, wote wanategemea mfumo uwabebe 4_4_2 au viungo bora wawabebe (pasi za mwisho mujarabu).Wote sio ma goal poacher,uwiano wa nafasi wanazotengeneza na magoli wanayofunga no tofauti Sana(wanatengeneza nyingi wanafunga machache). 

         Kabla ya hawa kuwepo Simba na Yanga kulikuwa Kuna washambuliaji waliowatangulia ambao nao walifanana kwa kiasi kikubwa ubora na mapungufu yao, 

     ATHUMANI MACHUPA na BONIFACE AMBANI .........Hawa walikuwa physical kawaida tu inayotosha kucheza mpira, tofauti kubwa na wenzako ni kuwa sifa ambazo kina KAGERE na MAYELE wanazo na wao wanazo Ila kina MACHUPA na mwenzie AMBANI wanawazidi wenzao mambo makubwa mawili,

   1.Mfumo kwao sio ishu Sana coz walikuwa na uwezo mkubwa binafsi,kumchukua beki mmoja wawili haikuwa tabu kwao.

 2.Hawa walikuwa goal poachers,mafundi Sana wa kutumia nafasi na wakati mwingine kutokana na uwezo binafsi walijitengenezea nafasi na kufunga magoli.

      Kufunga sio kazi ndogo, Ila Kuna misingi yake.Ni jukumu la makocha na wachezaji ku invest nguvu jitihada na weledi wa hali ya juu eneo Hilo.

   Nukuu ya nguli THIERRY HENRY ni kuwa kila baada ya mechi haijalishi kafunga 4,3,2 au hajafunga kabla hajaoga anairudia kuiangalia tena ile mechi na kubaini makosa aliyofanya ili ayafanyie kazi next matches............karibuni sana@mchambuzihuru.

Post a Comment

0 Comments