BETI NASI UTAJIRIKE

KICHUYA AWA GUMZO SIMBA,YANGA NA AZAM WAKIMPIGIA DORIA

Mshambuliaji hatari wa Namungo Shiza Ramadhan Kichuyahapo jana  amefunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanya aweze kufunga hat trick ya pili msimu huu.


Kichuya alifunga mabao hayo dakika ya 23, dakika ya 50 kwa mkwaju wa penalti na bao la tatu dakika ya 66 kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Bao lingine la Namungo lilifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 74, huku mabao ya  Mtibwa Sugar yakifungwa na Nzigamasabo Steve dakika ya 5 kwa mkwaju wa penalti na bao la pili likifungwa na George Makang’a dk ya 10.

Baadhi ya vilabu vimevutiwa na uwezo wake na kutamani waweze kumsajiliwa nyota huyo,Simba Yanga na Azam ni moja ya vilabu vinavyotajwa

Kwa msimu wa 2021/22 ni Jeremia Juma wa Tanzania Prisons alikuwa wa kwanza kufunga hat trick msimu mbele ya Namungo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

.

Post a Comment

0 Comments