BETI NASI UTAJIRIKE

ISHU YA MZAMIRU NA SIMBA IMEKAA HIVI

 Hatimaye kiungo punda wa Klabu ya Simba Mzamiru Yassin amelamba mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Kariakoo. Klabu huyo imefikia hatua hiyo baada ya nyota huyo kuwa nguzo muhimu kwa msimu wa 2021/22.


Mzamiru Yassin amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba na mkataba wake utamalizika mwaka 2024 mwezi juni. Nyota huyo alijiunga na Simba mwaka 2015 na ni moja ya wachezaji wakongwe wenye kiwango kizuri ndani ya timu hiyo.

Moja ya viongozi wa Simba alinukuliwa akisema 

Mzamiru amepewa mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga Simba, hiyo ni baada ya kazi yake kueleweka.Bado yupo ndani ya Sima hivyo wale ambao walikuwa wanahitaji saini yake wana kazi ya kuweza kuvunja mkataba na mabosi wa Simba.”

Post a Comment

0 Comments