Tetesi za ndani kabisa zinasema kuwa kocha huyo anaelekea kumaliza mkataba wake na miamba ya jangwani na mpaka sasa ameisaidia timu hiyo kutwaa kombe la ligi kuu NBC, kombe la Ngao ya jamii na sasa atacheza fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Coastal Union july 02.
Kuna uwezekano kocha wa Yanga Nabi Nasreddine akatua mitaa ya Simba msimu wa 2022/23 kama mrithi wa Pablo aliyetimuliwa klabuni hapo kwa mwenendo mbaya ndani ya Simba. Nabi amekuwa akihudhuria mechi mbalimbali za Simba na kuna uwezekano akatua klabuni hapo endapo hatapewa mkataba mpya na Yanga.Mkurugenzi mtendaji wa Simba Barbara Gonzalez amempongeza Nabi kwa kutwaa kombe la ligi kuu na ujumbe wake umezua hisia tofauti kwa mashabiki wa Yanga na Simba. Mpaka sasa Simba hawajamtangaza mrithi wa Pablo ingawa taarifa zinasema kocha mrithi atatua klabuni hapo hivi karibuni.
0 Comments