Klabu ya Yanga imetoa taarifa rasmi za kuachana na mchezaji wake raia wa Burundi Saido Ntabazonkiza. Mchezaji huyo aliyeitumikia miamba hiyo ya Jangwani ametimiza miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo na sasa anabaki kuwa mchezaji huru.
Siku ya Ijumaa klabu ya Yanga ilitoa taarifa rasmi ya kumsimamisha mchezaji huyo kushiriki mchezo dhidi ya Simba hatua ya nusu fainali kombe la Azam Sports Federation Cup kwa kuwa alitoroka kambini na alirejea siku inayofuata. Klabu hiyo kupitia msemaji wake Haji Manara ilisema watafanya naye mazungumzo mara baada ya mchezo na leo wametoa taarifa rasmi ya kuachana na mkongwe huyo
Historia Fupi ya Saido Ntabazonkiza ndani ya Yanga
Saido Ntabazonkiza alijiunga na klabu ya Yanga kama mchezaji huru mwaka 2020 na amecheza kwa mafanikio makubwa klabuni hapo akiisaidia kushinda mataji ya Ngao ya Jamii kwa msimu wa 2021/22 na lile la mapinduzi Cup kwa msimu wa 2020/21 pia amesaidia klabu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya ligi kuu na kuipeleka klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa na msimu huu ameisaidia klabu hiyo kucheza bila kufungwa ligi kuu NBC na FA kutinga fainali.
0 Comments