Hatimaye Klabu ya Wydad Athletic kutoka Morocco imefanikiwa kutwaa kombe la ligi ya mabingwa Afrika (CAF CHAMPIONS LEAGUE) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya bingwa mtetezi Al Ahly ya Nchini Misri mabao yakifungwa na Zaohair El Moutaraji dakika ya 15 kipindi cha kwanza na dakika 48 kipindi cha pili.
Wydad wameendelea kufanya vizuri pia ligi ya Morocco kwa kucheza michezo 24 wakishinda 16 sare 5 na kufungwa mechi 3 huku wakifungwa mabao 17 na kufunga mabao 20 wakijikusanyia pointi 53 na kuongoza kwenye msimamo wa ligi ya nchini humo
Mchezo Ulivyokuwa.
Al Ahly waliutawala mchezo huo kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza na walipiga mahuti 7 yaliyokwenda nje ya Uwanja. Mbali na kwamba Wydad walishindwa kulimiliki mpira dakika zote 45 lakini walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika 15 tu kwa shuti kali nje ya 18 lililopigwa na Moutaraji na kumshinda kipa wa Al Ahly huku wakipiga mipira minne nje ya goli
Kipindi cha pili Wydad waliumiliki mchezo huo kwa asilimia 56 na kupata bao la pili dakika ya 48 kupitia yule yule Moutaraji na kuwafanya wawe mabingwa kwa mara ya tatu wakifanya hivyo msimu wa 1991/92 ,2016/17 na sasa 2021./22
Hii inakuwa mara ya pili kwa Wydad kutwaa kombe hilo mbele ya Al Ahly baada ya kufanya hivyo msimu wa 2016/17 kwenye mchezo wa fainali ya raundi mbili ambapo mchezo wa kwanza ulipigwa Misri na ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1 na ule wa pili ulichezwa Morroco na ulimalizika kwa Wydad kushinda 1-0 na kuweka wastani wa wydad mabao 2-1 dhidi ya Al Ahly.
Historia Fupi ya Michuano.
Michuano hii ilianzishwa mwaka 1964/65 na Bingwa mara nyingi zaidi ni Al Ahly aliyetwaa kombe hilo mara 10 akifuatiwa na TP Mazembe pamoja na Zamalek wenye makombe 5 kila mmoja,Esperance Tunis wao wana makombe 4, Bingwa mpya Wydad Athletic wao wana makombe matatu sawa na Raja Club Athletic,Canon Younde na Hafia Football Club.
Ndani ya misimu 10 kocha Pitso Mosimane amefanikiwa kutwaa kombe hilo mara 3 akifanya hivyo ndani ya Al Ahly kwa makombe ya 2019./20 na 2020/21 huku aliipa Mamelodi Sundowns kombe hilo mwaka 15/16 na ndiye kocha pekee kucheza fainali 4 za Champions League na kutwaa ubingwa mara 3
1 Comments
Hongera WYDAD
ReplyDelete