advertise with us

ADVERTISE HERE

USIYOYAJUA KUHUSU FAINALI YA CAF LEO

Usiku huu wa leo tarehe 30 mei 30 2022I unakwenda kuweka historia mpya barani Afrika kwa kuzikutanisha klabu Mbili kubwa kwenye fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa saa 4 kamili usiku kwenye dimba la Stade Mohammed V nchini Morocco.

Mchezo huu mzuri na wakuvutia unaibua hisia zaidi kwa mashabiki wa Wydad ambao wanajukumu la kuvunja utawala wa Al Ahly aliyojiwekea kwa kucheza fainali ya 3 Mfululizo kwenye michuano hiyo huku akiwa na makombe 10 tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Kwa upande wa hapa nyumbani Mashabiki wa Simba watakuwa wakimuangalia aliyekuwa mchezaji wao tegemezi kwa msimu wa 2020/21 Luis Miquison waliyemuuza kwa mabingwa hao wa kihistoria Afrika

 

HISTORIA KWA UFUPI 

Michuano hii inazikutanisha timu 16 katika hatua ya makundi kutoka vyama vya Soka 56 Africa ambavyo hutoa timu 68 ambazo huchujwa hatua ya awali na kubaki timu 16 tu zinazounda makundi manne yenye timu 4 na zitacheza mechi sita kwa kila timu. Timu itakayoshika nafasi ya 1&2 huingia robo fainali na hatimae nusu fainali kisha fainali ambayo huchezwa  katika uwanja unaopangwa na CAF.

AL AHLY

Miamba hii ya Afrika ilifikia hatua hii baada ya kupangwa kundi A pamoja na Mamelodi Sundowns,Al Hilal na Al Merrikh na ilijikusanyia pointi 10 kwenye michezo 6 ikiwa nafasi ya 2 nyuma ya Mamelodi Sundowns aliyemaliza nafasi ya 1 akiwa na pointi 16 kati ya 18.

Robo Fainali ilicheza dhidi ya Raja Casablanca na kuibuka ushindi wa mabao 2-1 kwa mchezo wa raundi ya kwanza kusha sare ya 1-1 raundi ya pili.

Nusu Fainali walipangwa na ES Setif mchezo wa kwanza walishinda mabao 4-0 na mchezo wa pili walitoka sare ya 2-2 na sasa watakwaanza na Wydad AC ya nchini morocco kwenye mchezo wa fainali.

WYDAD AC 

Klabu hii ya Nchini Morocco imelishtua soka la Africa kwa msimu huu baada ya kuibuka na kinara wa kundi D kwa jumla ya pointi 15 wakishinda michezo 5 na kupoteza mmoja kwenye kundi lililojumuisha timu za Petro Luanda,Zamalek na Sagrada Esperence.

Hatua ya Robo fainali walicheza dhidi ya CR Belouizdad na mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Wydad kushnda ugenini kwa bao 1-0 na raumdi ya pili mchezo ulimalizika kwa sare ya mabao 0-0.

 Hatua ya Nusu fainali Wydad waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Petro Luanda na raundi ya pili waliibuka na sare ya 1-1 usiku huu watakutana na Bingwa mtetezi Al Ahly .

Kama Al Ahly atatwaa kombe hili kwa mara nyingine basi atakuwa ameweka rekodi ya kipekee sana kwenye michuano hii ya Afrika huku Kocha Pitso Mosimane atakuwa na rekodi ya kipekee kwa Soka la Afrika


Post a Comment

0 Comments