POLISI TANZANIA YAAMKA BIASHARA IKIPOTEZA MATUMAINI LIGI KUU

 Biashara United imeendelea kufanya vibaya ligi kuu NBC baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliochezwa uwanja wa Ushirika Moshi. Mabao ya Polisi Tanzania yaliwekwa kimiani na  Deus Dedith dakika ya 31 na Tariq Saif dakika ya 41 kipindi cha kwanza.

Matokeo hayo yanaifanya Biashara United kubakia nafasi ya 15 ikiwa na pointi 24 sawa na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 14 huku Mbeya Kwanza wakiendelea kubuluza mkia .

Polisi Tanzania wao wamesogea mpaka nafasi ya 07 kwenye msimamo wa ligi wakijikusanyia pointi 33 wakiiondosha Kagera Sugar yenye pointi 32 katika nafasi hiyo na sasa wanakibarua kigumu cha kuchukua nafasi ya Coastal Union aliye nafasi ya 6 akiwa na pointi 34 ,Geita Gold nafasi ya 5 akiwa na pointi 36 huku azam FC na Namungo wakiwa nafasi ya 3&4  na pointi 37.

Mpaka sasa ligi kuu NBC imezidi kuwa ngumu kwa kila timu huku Yanga wakiwa na uhakika wa kuchukua ubingwa na Simba ikiwa nafasi ya pili. klabu nyingine zinapambana kushikilia nafasi ya 3&4 ili ziweze kushiriki michuano ya CAF. 

Mpaka sasa hakuna timu inayoshuka daraja wala  kucheza Play OFF kwani timu zote zimekuwa zikiachana kwa pointi chache ilihali klabu za Ihefu na Singida Big Stars zimekwishapanda Daraja wakati Kitayose na JKT Tanzania zikingoja mchezo wa Play OFF

Post a Comment

0 Comments