BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 21 APRIL 2022

 Real Madrid wana uhakika wa kumsajili Kylian Mbappe, 23, na watafanya kila wawezalo kumpata mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain na Ufaransa baada ya kukubali kwamba mlengwa wao mkuu, Erling Braut Haaland, anaelekea Manchester City.(Mail)


Real pia wana nia ya kumleta kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham huko Bernabeu, lakini Borussia Dortmund wanatamani sana kusalia na kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 na wananuia kuongeza msimamo wake ndani ya uongozi wa klabu hiyo katika jaribio la kumshawishi chipukizi huyo kusalia. (Bild - kwa Kijerumani)

Everton inamfuatilia Adama Traore ,26, wa Wolves kwa nia ya kumsajili winga huyo wa Uhispania ikiwa Barcelona itakataa chaguo la kufanya uhamisho wake wa mkopo Nou Camp kuwa wa kudumu. (Football Insider)

Adama Traore

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha

Kocha anayekuja wa Manchester United Erik ten Hag atakuwa na £200m za kutumia kununua wachezaji wapya, huku wachezaji sita wa kikosi cha kwanza wakitarajiwa kuondoka katika msimu wa joto. (Mirror)

Anthony Martial huenda akarejea Old Trafford baada ya kuchezea Sevilla kwa mkopo wa msimu mzima kwa sababu klabu hiyo ya Uhispania haijaanzisha mazungumzo ya kusalia na Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 26. (Fabrizio Romano)Wawakilishi wa Paul Pogba wanafanya mazungumzo na Juventus na Real Madrid kuhusu uhamisho wa majira ya joto, wakati kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 atakapokuwa mchezaji huru. (Sky Sports)

CHANZO CHA PICHA

Meneja wa Tottenham Antonio Conte yuko tayari kufanya mazungumzo na Daniel Levy kumwambia mwenyekiti wa Spurs kwamba klabu hiyo inahitaji kuwasajili wachezaji sita msimu wa joto, huku kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 24, akiwa juu kwenye orodha. (Telegraph - usajili unahitajika)

Tottenham pia wanamsaka beki wa kulia wa Uingereza Djed Spence, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Nottingham Forest kutoka Middlesbrough. (Mail)

Spurs itamsajili winga wa Uswidi Dejan Kulusevski kwa mkataba wa kudumu katika majira ya joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 yuko amekuwa nao kwa mkopo wa miezi 18 na Tottenham wameamua kulipa Juventus ada ya pauni milioni 24.9 msimu huu. (Evening Standard)

Dejan Kulusevski

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Winga wa Ureno Fabio Carvalho, 19, amesema nia ya Liverpool ya kutaka kumsajili imeathiri kiwango chake cha mchezo hivi majuzi huko Fulham. (Metro)

Ivan Toney anataka mkataba mpya na nyongeza ya mishahara huko Brentford, ambako mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 yuko chini ya mkataba hadi 2025. (90 Min).

Wachezaji wa ulinzi wa Torino, Mbrazil Gleison Bremer, 25, na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Singo, 21, wanalengwa na mkurugenzi wa soka wa Tottenham Fabio Paratici. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Leeds na Everton wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Besiktas. (TeamTalk)

West Ham wanavutiwa na winga wa Club Bruges Noa Lang, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 22. (Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)

Post a Comment

0 Comments