BETI NASI UTAJIRIKE

NAMUNGO WAJIPANGA KUIHARIBIA YANGA JUMAMOSI

 Klabu ya Namungo imeendelea kujipanga kisawasawa kuelekea mchezo wa ligi kuu NBC dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa tarehe 23 jijini Dar es Salaam. Namungo yenye makao yake makuu mkoani Lindi imeendelea na mazoezi yake ya mwisho jioni ya leo katika uwanja wake wa nyumbani ILULU STADIUM.



Kikosi hicho kitaanza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam hapo kesho asubuhi.Mpaka sasa kikosi hicho chenye wachezaji wawili waliowahi kuitumikia Yanga ambao ni Obray Chilwa na David Molinga kipo kamili na hakuna mchezaji yeyote mwenye tatizo la kiafya.

Namungo wanashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 29 kwenye michezo 20 waliyocheza. Klabu hiyo kwa sasa inapambana kushika nafasi nne za juu ili iweze kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika au Kombe la Shirikisho na hiyo inachochea wachezaji hao kujituma zaidi kwenye mchezo huo.

Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji hao wakifanya mazoezi ya mwisho

Post a Comment

0 Comments