MUDA WA SHOW ZA CHAMA, LWANGA NA WAWA NDIO HUU

 Mchezaji bora wa Mwezi Machi Ligi kuu NBC Clatous Chota Chama leo hii anarejea uwanjani tena kuisaidia timu yake ya Simba kutetea kombe la ligi kuu dhidi ya Coastal Union mchezo wa raundi ya 18 kwa SimbaChama alikuwa gumzo kwa mwezi wa tatu baada ya kufunga mabao 4 na kutengeneza mawili na tangu kurejea kwake mwezi january kutoka RS Berkane ya Morocco amekuwa akionyesha kiwango kilekile alichokuwa nacho kwa msimu wa 2020/21 na kumfanya awe kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Simba.

Kwa msimu huu Chama atashiriki michuano ya ndani tu ikiwa na maana ya ligi kuu NBC na Azam Sports Federation Cup na hatacheza mchezo wowote wa michuano ya CAF kutokana na kuitumikia klabu ya RS Berkane inayoshiriki michuano hiyo mwanzoni mwa msimu wa 2021/22

Chama amekuwa ni moja ya nyota muhimu kwa klabu ya Simba na leo hii atacheza sambamba na Bernad Morrison,Chriss Mugalu ,Kibu Denis na Kanoute ambao wataongoza safu ya ushambuliaji ya Simba huku Wawa,Kapombe Onyango Tshabalala na Lwanga. 

Tadeo Lwanga amekosekana kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha kwanza kutokana na majeraha huku Pascal wawa akipata wakati mgumu wa kurejesha namba yake kikosini kutokana na ubora wa Inonga tangu ajiunge na miamba hiyo ya msimbazi

Post a Comment

0 Comments