Ukiwa unatazama mechi za Yanga basi kila utakaposkia jina la Mayeleee basi jua mpira upo wavuni au kipa ameachwa na hali mbaya kwa kuokoa mashuti ya Straika huyu hatari kutokea nchini Congo.
Mayele alijiunga na Klabu ya Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2021/21 akitokea klabu ya AS Vita ya nchini Congo. Tangu kuwasili kwa mchezaji huyo klabu ya Yanga imekuwa tishio kwa kila timu inayokutana nayo. Hakuna cha Simba ,Azam wala Kagera Sugar aliyowaacha Salama.
Mpaka sasa nyota huyo amekwishafunga jumla ya mabao 11 kwenye mechi 16 alizocheza ligi kuu huku akitengeneza mengine 3. na kumfanya kuwa na wastani wa 0.8 kwenye kila mechi ya ligi anayocheza.
Mayele amekuwa mwiba mkali kwa mabeki visiki kuanzia Joash Onyango mpaka kwa mkongwe Agrey Morris ambapo kwa mechi ya jana kati ya Yanga na Azam tulishuhudia beki huyo mkongwe akipata kashikashi nyingi na mwisho wa siku alikubali yaishe na Mayele kupata bao la pili kwenye mchezo huo.
Kwa miaka minne mfululizo sikuwahi kumshuhudia straika wa kiwango cha Mayele akiichezea Yanga. Mastraika wliopita kama David moringa,Michael Sarpong ,Yikpe na Tarik hauwezi hata kidogo kuwalinganisha na anachokifanya Mayele kwa sasa. Uwezo wake unaifanya klabu ya Yanga kujiamini kutwaa kombe ligi kuu na FA ambayo wameyakosa kwa muda mrefu.
Kinachomfanya Mayele awe tishio ni uwezo wa kufunga kwa staili zote kuanzia kichwa ,mguu wa kushoto na kulia na hizo tiki taka zake ndio zinazotisha zaidi. Meddie Kagere,John Bocco,Laurent Lusajo na Chris Mugalu ni baadhi ya mastraika hatari wanaocheza ndani ya ligi yetu ambao wameweka rekodi kubwa sana kwa misimu iliyopita ila kwa msimu huu Fiston Mayele ni baba lao NBC Premier League
0 Comments