KWA SIMBA HII ORLANDO PIRATES WATAPIGWA PALEPALE KWA MANDELA

 Klabu ya Simba imeendelea na mazoezi makali jioni ya leo kuelekea mchezo wa pili wa robo fainali utakaopigwa jumapili ya tarehe 24 dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini. Klabu hiyo imezidi kujiimarisha zaidi kuelekea mechi hiyo baada ya wachezaji wake wawili Joash Onyango na Sadio Kanoute kumaliza adhabu ya kadi.


Jambo kubwa ni mipango thabiti waliyojiwekea kwenye mchezo huo. Baadhi ya wadau wa soka wanaamini mchezo huo utakuwa mwepesi sana kwa Simba tofauti na ule wa raundi ya kwanza kwani Simba watacheza kwa umakini wakiwa hawana Presha tofauti na Orlando Pirates ambao wana deni la bao moja.

Kocha Pablo ataongoza kikosi hicho kuelekea Afrika Kusini na haijawekwa wazi ni lini timu hiyo itatua Afrika Kusini kupambana na Maharamia hao wa Baharini ilihali mchezo wao utapigwa siku ya jumapili.

Hizi ni baadhi ya picha Simba wakijiandaa na mchezo huo katika dimba la Bunju
Post a Comment

0 Comments