JESHI LA NABI LIPO TAYARI KUISAMBARATISHA NAMUNGO JUMAMOSI

 Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi makali kuwakabili wapinzani wao Namungo kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa jumamosi ya tarehe 23 dimba la mkapa jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 51 kwenye michezo 19 waliyocheza na ushindi wa mchezo huo utachochea mbio za ubingwa.


Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Nabi na msaidizi wake Kaze kimeendelea na mazoezi makali jioni ya leo katika viwanja vya Avic Town kigamboni na uuzwaji wa tiketi umeendelea katika vituo mbalimbali.

Habari njema ni kuwa Yanick Bangala,Khalid Aucho na Feitoto wamesharejea mazoezini na watapangwa kwenye mchezo huo.

Hizi ni baadhi ya picha za  mazoezi Post a Comment

0 Comments